Uislamu kwa nchi

Uislamu ni dini ya pili duniani kwa wingi wa wafuasi. Kulingana na utafiti uliofanywa mwaka 2010 na kutolewa Januari 2011, Waislamu ni bilioni 1.57, unachukua zaidi ya asilimia 23 ya idadi ya watu wote. Waislamu walio wengi ni wa madhehebu ya: Sunni (75–90%) au Shia (10–20%). Ahmadiyya wanawakilisha karibia 1% ya Waislamu wa dunia nzima. Uislamu ni dini yenye nguvu huko Mashariki ya Kati, Afrika Magharibi, Pembe la Afrika, Sahel, na baadhi ya sehemu za Asia. Baadhi ya jumuia za Kiislamu pia zinapatikana huko Uchina, Balkans, Uhindi na Urusi. Sehemu nyingine za dunia ambazo zina jumuia nyingi za wahamiaji wa Kiislamu ni pamoja na Ulaya ya Magharibi, kwa mfano, ambapo Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa baada ya Ukristo, ambapo inawakilisha asilimia 6 ya jumla ya wakazi wote. Kulingana na ripoti ya Pew Research Center mnamo 2010 kulikuwa na idadi kubwa ya Waislamu katika nchi zipatazo 49. Karibu asilimia 62 ya Waislamu wa duniani kote wanaishi Kusini na Kusini mashariki mwa bara la Asia, ikiwa na wafuasi zaidi ya bilioni 1. Nchi yenye idadi kubwa ya Waislamu duniani ni Indonesia, hii peke yake inachukua asilimia 12.7 ya idadi ya Waislamu wote wa dunia, ikifuatiwa na Pakistan (11.0%), India (10.9%), na Bangladesh (9.2%). Karibia asilimia 20 ya Waislamu wanaishi katika nchi za Kiarabu. Huko Mashariki ya Kati, nchi ambazo si za Kiarabu - Uturuki na Iran - ni nchi zenye Waislamu wengi sana; huko Afrika, Misri na Nigeria zina jumuia nyingi za Kiislamu. Utafiti huo umekuta Waislamu wengi zaidi huko Uingereza kuliko hata Lebanon na wengi zaidi huko China kuliko hata nchini Syria.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search